JOHN 14

Tuesday, 25 December 2012

Askofu apinga ndoa ya wapenzi wa jinsi moja

Kiongozi wa Kanisa wa Katoliki nchini Uingereza amesema mpango wa serikali ya Uingereza kuhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja ni jambo la aibu.

Askofu mkuu wa Jimbo wa Westminster Vincent Nichols ameiambia BBC kuwa serikali ya Uingereza haina wajibu wa kuhimiza ndoa ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza.

Katika hotuba yake wakati wa misa ya Krismasi, askofu Nichols alisema ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inaashiria mapenzi ya Mungu.
Serikali ya Uingereza inapanga kuruhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja lakini imesema kuwa haitawashurutisha viongozi wa dini kuongoza na kuidhinisha ndoa hizo.

Kwingineko, Askofu wa jimbo ya Centerbury anayeondoka, Rowan Williams amesema heshima na hadhi ya Kanisa la Kianglikana na nchini Uingereza, limeadhirika pakubwa kutokana na uamuzi wa hivi majuzi ambao ulipinga uteuzi wa kina mama kama askofu wa kanisa hilo.

Dr Williams anatarajiwa kustaafu kutoka wadhifa huo mwisho wa mwezi huu.

Sunday, 11 November 2012

Askofu ataka wacheza kamari watoe sadaka

Askofu Justin Welby, aliyeteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, yaani Askofu wa Canterbury, amependekeza kwenye mtandao wa Twitter kwamba mtu yeyote aliyeshinda kwenye kamari kwa kubahatisha kuwa yeye ndiye atateuliwa, anafaa kutoa fedha hizo kama sadaka kwa kanisa.


Mwanzo wa juma hili makampuni ya kamari yalitangaza kuwa yamesimamisha kamari juu ya nani atakuwa kiongozi mpya wa kanisa la Anglikana, kwa sababu wengi walifikiri kuwa ni Askofu Welby, ambayo inaonesha baadhi ya maafisa wakijua kuwa jina hilo ndilo lilopendekezwa.

Askofu Welby atachukua nafasi ya Rowan Williams mwaka ujao kuwa kiongozi wa wamumini wa Kianglikana dunia nzima.

Saturday, 10 November 2012

KANISA LA ANGLICAN LAPATA ASKOFU MKUU MPYA Cantebery



Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa kanisa hilo , Justin Welby amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.
Taarifa zinazohusiana
Uingereza
Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti. Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Nigeria, Nichola Okoh, ameimbia BBC kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja usitetewe na Kanisa.