JOHN 14

Tuesday, 25 December 2012

Askofu apinga ndoa ya wapenzi wa jinsi moja

Kiongozi wa Kanisa wa Katoliki nchini Uingereza amesema mpango wa serikali ya Uingereza kuhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja ni jambo la aibu.

Askofu mkuu wa Jimbo wa Westminster Vincent Nichols ameiambia BBC kuwa serikali ya Uingereza haina wajibu wa kuhimiza ndoa ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza.

Katika hotuba yake wakati wa misa ya Krismasi, askofu Nichols alisema ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inaashiria mapenzi ya Mungu.
Serikali ya Uingereza inapanga kuruhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja lakini imesema kuwa haitawashurutisha viongozi wa dini kuongoza na kuidhinisha ndoa hizo.

Kwingineko, Askofu wa jimbo ya Centerbury anayeondoka, Rowan Williams amesema heshima na hadhi ya Kanisa la Kianglikana na nchini Uingereza, limeadhirika pakubwa kutokana na uamuzi wa hivi majuzi ambao ulipinga uteuzi wa kina mama kama askofu wa kanisa hilo.

Dr Williams anatarajiwa kustaafu kutoka wadhifa huo mwisho wa mwezi huu.

Sunday, 11 November 2012

Askofu ataka wacheza kamari watoe sadaka

Askofu Justin Welby, aliyeteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, yaani Askofu wa Canterbury, amependekeza kwenye mtandao wa Twitter kwamba mtu yeyote aliyeshinda kwenye kamari kwa kubahatisha kuwa yeye ndiye atateuliwa, anafaa kutoa fedha hizo kama sadaka kwa kanisa.


Mwanzo wa juma hili makampuni ya kamari yalitangaza kuwa yamesimamisha kamari juu ya nani atakuwa kiongozi mpya wa kanisa la Anglikana, kwa sababu wengi walifikiri kuwa ni Askofu Welby, ambayo inaonesha baadhi ya maafisa wakijua kuwa jina hilo ndilo lilopendekezwa.

Askofu Welby atachukua nafasi ya Rowan Williams mwaka ujao kuwa kiongozi wa wamumini wa Kianglikana dunia nzima.

Saturday, 10 November 2012

KANISA LA ANGLICAN LAPATA ASKOFU MKUU MPYA Cantebery



Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa kanisa hilo , Justin Welby amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.
Taarifa zinazohusiana
Uingereza
Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti. Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Nigeria, Nichola Okoh, ameimbia BBC kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja usitetewe na Kanisa.

Sunday, 24 July 2011

BABA ASKOFU ABARIKI UJENZI

ASKOFU MKUU WA KANISA LA ANGLIKAN TANZANIA VALENTINO MOKIWA ABARIKI UJENZI WA KANISA MARA BAADA YA KUJA KUSHUHUDIA UJENZI WA KANISA JIPYA LA MTAA WA MICHAEL LILIPO KUNDUCHI MTAKUJA PEMBENI NI MOJA YA WAZEE WA KANISA MZEE MGWENO.

KULIA HAPA NI BABA PADRI KOMBA  PADRI WA MTAA NA ASKOFU WAKITAZAMA KAZI YA UJENZI WA KANISANI INVYOEENDELEA -

Thursday, 9 June 2011

HAYA NDIO MAENDELEO YA UJENZI WA KANISA ANGLIKANA KUNDUCHI !





 HII PICHA INAYONYESHA KANISA LA ANGLIKANA KUNDUCHI KARIBU KABISA NA SHULE YA MSINGI MTAKUJA KWA MBELE IKIONYESHA MAENDELEO YA UJENZI YANAVYONDELEA KUJENGA NYUMBA YA KUMSHUKURU .




HAPA NI MUONEKANO WA MBELE KWA JUU LIKIONYESHA MADHABAHU  ITAKAVYOKUWA IKIONEKANA .



 
MUONEKANO HUU NI WA PEMBENI WA KANISA HILI UKWELI NI KWAMBA WAMEDHAMILIA KUJENGA  HILI AMBALO LITAWEZA KUCHUKUA WAAMUNI ZAIDI YA MIA MOJA KWA MISA .


HII NI PICHA INAYOONYESHA KANISA HILI NYUMA JINSI LINAVYOJENGWA KWA USTADI WA HARI JUU MUNGU AWABARIKI SANA WANAOJENGA KANISA HILI.

HII NI MOJA KATI YA SEHEMU AMBAZO ZINARAJI KUMALIZIKA PUNDE MARA BAADHI YA MAMBO YA KAMATI YA UJENZI YATAKAPO KAMILIKA

Thursday, 25 June 2009

KANISA ANGLIKANA WAMEANZA KAZI UNAONA WANAWEKA JANVI

Unaona mafundi wanavyochapa kazi kwa kweli inawezekana Mafundi wakiweka sawa sehemu ya madhabahu ya bwana
Pastor akiwajibika kujenga kanisa hii ni kazi ya mungu jamani


Moja kati ya mafundi wakimwaga zege ilikukamilisha moja kati ya hatua za kwanza za ujenzi wa kanisa


Mafundi wakianza kutemgeneza sehemu ya kusomea matangazo kule juu madhabauni janzi limeanza kukauka








Tuesday, 23 June 2009

HAKUNA LISILO WEZEKANA

Chini ni mchoro wa ramani ambao utatumika katika ujenzi wa kanisa la st Michael kunduchi.
Chini Father Rev Richard kamenya akitafakari jambo na mwinjilisti Michael Ndawile okroro Father kwa kamenya kwa sasa amepata uhamisho na ansalisha kanisa la anglikana makuburi.

Chini ni wana kwaya wa kanisa la st Michael wakitazama ufundi wa upiga picha za video unaofanywa na Juma kazimoto.